Isaya alikuwa ni nabii aliyeishi karibu miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo hapa duniani. Pamoja na kuwa alitangulia kabla ya kuja kwa Yesu Kristo kwa miaka 700, na kwa sababu alifahamu mambo mengi kuhusu Masihi, Isaya alitabiri yote kuhusu jinsi Masihi atakavyokuja na jinsi atakavyofanya kazi yake ya wokovu kana kwamba alimuona Masihi kwa macho yake mwenyewe. Ukianzia Isaya 52:13 na kuendelea sura za 53 na 54, Isaya aliendelea kutabiri, kwa wazi na kwa kina, juu ya jinsi ambavyo Masihi atawaokoa wanadamu kutoka katika dhambi. Ni jambo la kushangaza sana kwamba Isaya alitabiri kwa usahihi kabisa kuwa Yesu Kristo atakuja hapa duniani na kuzichukua dhambi zote katika ubatizo wake, na kuimwaga damu yake Msalabani na hivyo kuuleta wokovu kwa wote. Na baada ya miaka 700 kupita tangu Isaya alipoutoa unabii wake, Yesu Kristo alikuja hapa duniani na akazitimiza kazi zake zote kwa usahihi kama ilivyotabiriwa na Isaya.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Mungu alimwamuru Musa kwenda juu katika Mlima Sinai na akampatia mtitiriko mzima wa Sheria yake. Kwanza kabisa, alimpatia Musa Amri Kumi: “Usiwe na miungu...
Kifungu kikuu cha maandiko kinatoka katika Kutoka 19:1-6. Japokuwa kifungu hiki cha maandiko si kirefu, nina mambo mengi ya kuzungumza kuhusu kifungu hiki. Kutoka...
Hebu tuanze kwa kuangalia Kutoka 3:13-16: “Musa akamwambia Mungu, ‘Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao...